MOURINHO: "BADO USAJILI WA MCHEZAJI MMOJA"
Mashetani Wekundu wamechezea kichapo cha 4-1 kutoka kwa Borussia Dortmund na Jose Mourinho amesisitiza bado ataendelea kusajili kuimarisha kikosi
Bosi wa Manchester United, Jose Mourinho amethibitisha kuwa Mashetani Wekundu bado wanatafuta kiungo wa kati ili kukamilisha biashara yao ya usajili tayari kwa msimu mpya.
Eric Bailly, Henrikh Mkhitaryan na Zlatan Ibrahimovic wamewasili Old Trafford msimu huu wa majira ya joto na kuna uwezekano mkubwa wa kiungo wa Juventus Paul Pogba kuwa mchezaji wa mwisho kusajili na wa Jose Mourinho.
Mreno huyo amethibitisha kuwa bado mchezaji mmoja zaidi atasajiliwa kabla ya kufungwa dirisha la usajili, amesisitiza kuwa biashara hiyo itafanyika kutokana na mambo yasiyotarajiwa yatakayotokea katika kipindi cha maandalizi.
"Tunashawishika kabisa kuhusu uwezo wetu wa kushughulika na soko. Lengo letu ni wachezaji wanne. Mmoja kiungo wa kati, mmoja beki, mmoja mshambulizi na mwingine mchezaji mbunifu, na tutakapomaliza biashara hiyo tutakuwa tupo kamili" Mourinho aliwaambia waandishi.
"Leo hatukuwa na Ibrahimovic, wala Fellaini, wala Martial, wala Schneiderlin. Kwahiyo nafasi zao hazikuwepo. Soko lipo wazi hadi Agosti 31 na wakati mwingine mambo hutokea isivyotarajiwa na ni sharti utende kulingana na hali halisi. Lakini tuna asilimia 75, na tutakaposajili kiungo wa kati mmoja, kazi muhimu itakuwa imekamilika."
Mourinho ameongea na vyombo vya habari kufuatia kipigo cha Ijumaa cha 4-1 kutoka kwa Borussia Dortmund huko Shanghai.
Chanzo: goal
No comments:
Post a Comment