Mahakamani-Uganda: Kizza Besigye Aachiwa kwa Dhamana
The Forum for Democratic Change (FDC)
The Forum for Democratic Change (FDC)
The Forum for Democratic Change (FDC)
Kizza Besigye Kifefe aliyekuwa akishikiliwa tangu
mwezi Mei mwaka, 2016 akituhumiwa kwa kosa la uhaini.
Aidha jaji wa mahakama amemtaka Besigye
kujiepusha na matukio ya vurugu na kuhakikisha katika jamii amani
inatawala. Pia ametakiwa kila baada ya wiki mbili kuanzia Julai 26
atatakiwa kuripoti kwa msajili wa mahakama.
Awali, mwanasheria wa serikali, Florence
Akello aliitaka mahakama kutompa Besigye dhamana kwani hakuwa ameleta
nyaraka halali zinazoonyesha tarehe yake ya kuzaliwa na kuwa ana umri wa
miaka 60. Lakini jaji alitupilia mbali ombi hilo kwa maelezo kuwa,
mwanasheria huyo pia hakuwa ameleta nyaraka zinazoonyesha kuwa mtuhumiwa
hana miaka 60.
Baada ya maamuzi hayo ya mahakama, wafuasi wa Besigye waliimba wimbo wa taifa huku taratibu nyingine za kuachiliwa zikifuata.
Source: News Vision-Uganda
No comments:
Post a Comment