MENU

Tuesday, September 6, 2016

Je wajua? Betri za Lithium hulipuka



Uamuzi wa kampuni ya simu ya Samsung wa kusitisha mauzo ya simu mpya ya Galaxy Note 7 kutokana na ripoti za kulipuka kwa betri zake ni hatua isiyokuwa ya kawaida kwaa kampuni kubwa ya kiteknolojia.  Kampuni hiyo imesema kuwa imebaini kasoro iliopo katika betri hizo lakini haikutoa maelezo zaidi. Lakini iwapo Betri ya Lithium-ion inashika chaji haraka ni hatari sana kunapotokea kasoro kwa sababu huenda ikasababisha moto. Kumekuwa na visa 35 vya Galaxy Note 7 kushika moto duniani baada ya mauzo ya takriban simu milioni 2.5,kulingana na Samsung. Betri za Lithium zinazotumika na Samsung hutumika sana katika viwanda vya kiteknolojia-Lakini ni nini inachozifanya kuwa hatari?.

No comments: