Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi) Dkt. Leornard Chamuriho amesema maandalizi yote kwa ajili ya uzinduzi wa ndege hizo yamekamilika na uzinduzi huo utafanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Kesho kuanzia saa mbili asubuhi. “Tunawaomba wanahabari na wananchi kujitokeza kwa wingi katika uzinduzi huo ili waone utekelezaji wa ahadi wa Serikali katika mkakati wa kuhuisha usafiri wa Anga hapa nchini”, amesema Dkt. Chamuriho.
No comments:
Post a Comment