- Trump sasa anaamini Obama alizaliwa Marekani
- Kinywaji cha ''kupoteza ubikira'' chazua mjadala China
- Madereva wa malori wa Tanzania na Kenya waliotekwa DR Congo waokolewa
- Chatu mwenye urefu wa futi ishirini ameuawa kwenye shamba la Rais wa Uganda Yoweri Museveni eneo la Kisozi lililo wilaya ya Gomba.
- Raia wako huru kutumia fedha zao kidogo ili kupata huduma ya choo kilichotengezwa na dhahabu katika jumba la makumbusho la Guggenheim. Msanii kutoka Italy,Maurizio Cattelan alijenga choo hicho kwa kutumia carat 18 za dhahabu na kukiita choo hicho Marekani.
- Malaysia imethibitisha kuwa kipande cha ndege kilichopatikana Pwani ya kisiwa cha Pemba, Visiwani Zanzibar nchini Tanzania mwezi Juni mwaka huu, ni ya ndege ya abiria iliyotoweka ya MH370 mwaka 2014.
- Umoja wa Mataifa watishia kuiwekea vikwazo Sudan Kusini
- Rais wa zamani wa Israel na kiongozi aliyetunukiwa tuzo ya Amani ya Nobel Shimon Peres, mwenye umri wa miaka 93, amelazwa hospitalini kwa dharura Jumanne usiku karibu na mji wa Tel Aviv na kupatishiwa msaada wa vifaa vya kumsaidia kupumua baada ya kupatwa na kiharusi, ofisi yake imearifu katika taarifa yake.
- Rais wa Zambia Edgar Lungu ameapishwa kuongoza nchi hiyo kwa muda wa miaka mitano ijayo baada ya kutangazwa mshindi katika Uchaguzi Mkuu wa mwezi Agosti mwaka huu.
- Kamishna mkuu wa Haki za Binadamu katika Umoja wa Mataifa, Zeid Ra'ad Al Hussein, amelaumu Jumanne hii kwamba nchi nyingi zimekataa kushirikiana na wataalam wake na waangalizi wa kimataifa, akilaumu hasa Syria, Iran na Venezuela.
- Wasanii wanaoshiriki kwenye tamasha la Fiesta, wamechangia shilingi milioni 40 kusaidia waathirika wa tetemeko la ardhi lililosababisha vifo na kuharibu makazi ya maelfu ya wananchi hususan mkoani Kagera.
- “Kuna maeneo anafanya vizuri, kuna maeneo ambayo naamini tungefanya vizuri zaidi, hili niishie hapo, anafanya vizuri kiasi gani ameshindwa kiasi gani tuwaachie wataalamu wengine wachambue”, alisema Lowassa. Ameyasema hayo katika mahojiano maalumu na ripota wa BBC mjini Nairobi na aliweza kujibu maswali kadhaa. Moja ya maswali hayo ni pamoja na anavyouchukulia utendaji wa Dkt Magufuli.
- MAHAKAMA ya Rufani imemhukumu kunyongwa hadi kufa aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Kinondoni (OC-CID), Mrakibu wa Polisi (SP) Christopher Bageni, baada ya kumtia hatiani kwa kosa la mauaji ya watu watatu. Aidha imemuachia huru aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Dar es Salaam (RCO) Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Abdallah Zombe na maofisa wengine wawili wa Polisi, Ahmed Makelle na Rajabu Bakari, baada ya kuwaona hawana hatia.
- WANAFUNZI wa Kidato cha Sita Shule ya Sekondari Usevya wilayani Mlele Mkoa wa Katavi, wanadaiwa kuwashambulia kwa kuwacharaza viboko walimu wao wawili miongoni mwao akiwemo Makamu Mkuu wa Shule hiyo, Makonda Ng’oka “Membele'‘ (34) ambaye ameng’olewa meno matano kwa kipigo hicho.
No comments:
Post a Comment