MENU

Tuesday, July 12, 2016

TIBA ASILIA: Serikali yamfungia Dr. Mwaka







Serikali imefungia kituo cha tiba asilia cha Foreplan kinachomilikiwa na Tabibu Juma Mwaka Juma kwa kukiuka masharti ya kibali alichopewa kwa kujitangaza kuwa anatoa tiba za kisasa badala ya matibabu ya asilia.

Baraza la Tiba Asili na Tiba limesema kuwa kituo hiko kimefutiwa usajili na hakiruhusiwi kutoa huduma za tiba asilia na Tiba mbadala kwa jamii
. Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, Mwenyekiti Wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala, Dk Edmund Kayombo amesema kuwa kituo hiko kimefutiwa usajili na hakiruhusu kutoa huduma za tiba asilia na tiba mbadala kwa jamii kwa kutokidhi masharti ya usajili na kufanya kazi kinyume cha usajili wake.

                                                  Dr. Mwaka akiwa na msanii Diamond

No comments: