PICHA: Kituko cha Rais Museveni leo
Rais Yoweri Museveni wa Uganda amekuwa gumzo leo kwenye mitandao ya kijamii. Hiyo ni baada ya picha zake kuzagaa akiwa pembezoni mwa barabara aliposimamisha msafara wake katika kijiji cha Kyeirumba ili aongee na simu muhimu huku akiwapungia wananchi. Raisi Museveni alikuwa anaelekea Wilaya ya Isingiro baada ya kuhudhuria Sherehe za Siku ya Idadi ya Watu Duniani (World Population Day). Wananchi hao waliishukuru serikali kwa kuweka barabara ya lami inayounganisha nchi hiyo na Tanzania kupitia Isingiro. Barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 74 iligharimu shilingi milioni 178 za Uganda. Pia, wananchi hao waliiomba serikali kuwapunguzia kodi wasambazaji wa vifaa vya umeme wa jua ili wapunguze gharama za usambazaji. Raisi Museveni alaiahidi kulishughulikia ombi lao.
No comments:
Post a Comment