MENU
Thursday, November 3, 2016
Wednesday, November 2, 2016
Africa Kusini: Maandamano yanaendelea muda huu
Kiongozi wa Chama cha EFF, Julius Malema anaendesha maandamano
leo yasiyo na kikomo ili kumng'oa madarakani Rais Zuma. Wanashinikiza Rais Zuma ajiuzulu sababu ya kashfa za Ufisadi
zinazomkabili. Baadhi ya barabara zimefungwa katika jiji la Pretoria. Maandamano hayo yasio na kikomo yameanzia Church Square katikati ya jiji la
Pretoria. Julius Malema akiwa anawahutubia wafuasi wake mbele ya
Mahakama Kuu Pretoria aliwaambia kuwa maandamano yatamaliza pindi
watakapojisikia kuondoka, lakini hawatakuwa na nia hiyo ya kuondoka. Na pia amewahataadharisha Polisi kutoingilia maandamano yao, amewaambia
kazi yao ni kuhakikisha wanapatiwa usalama na si vinginevyo. Amesema
hana haja ya kuomba kibali cha maandamano kutoka Polisi au Mahakamani
kwani ni haki yake kisheria.
Hapo awali, Malema aliwaambia Polisi yeye kama Julius Malema Kazi yake nikuandaa Maandamano na kuhakikisha yanafanyika na Polisi kazi yao ni kuwalinda.
Maandamano yameanza rasmi leo tarehe 2016 November 02 kuanzia saa 12 za
asubuhi mpaka hapo Zuma atakapo achia nchi. Amesema uhuru wa Afrika Kusini haukupatikana kirasihi halafu yeye Zuma
aje waibie rasilimali zao, wakati watu wengi waliuwawa kupigania uhuru.
Mahakani Kinondoni: Lady Jay Dee Apatikana na Kosa
Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni yamuamuru Judith Wambura (Lady Jay Dee) kumuomba msahama Joseph Kusaga & Ruge Mutahaba kwa kumkashifu. Je, Komandoo huyu ataomba msamaha hadharani kama alivyotakiwa? Fuatilia Blog hii kwa habari zaidi....!
Breaking News: Chuo cha Makerere Chafungwa
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Makerere Uganda kimefungwa baada
ya Rais Museveni kukifunga kwa muda sababu ya mgomo wa wahadhiri na wanafunzi kwa kuhofia uharibifu wa miundombinu ya chuo hicho.
Madini Mapya yangundulika Tanzania
Madini mapya yamegunduliwa nchini Tanzania, katika eneo lenye madini ya kipekee la Manyara, na kupewa jina Merelaniite. Jina
hilo limetokana na eneo ambalo madini hayo yalipatikana, Merelani
(Mererani) katika milima ya Lelatema katika wilaya ya Simanjiro katika
eneo la Manyara. Eneo hilo linafahamika sana kwa madini ya Tanzanite. Madini
hayo yaligunduliwa na wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Kiteknolojia cha
Michigan cha Marekani, makavazi ya historia asilia ya London, chuo kikuu
cha Di Firenze cha Italia na makavazi ya historia asilia ya Smithsonian
ya Washington.Wataalamu sita waliofanya uchunguzi, kwenye makala
iliyochapishwa kwenye jarida la Minerals (Madini) wanasema madini hayo
yana vipande vinavyofanana na sharubu vya rangi ya kijivu vya urefu wa
milimita moja hivi, ingawa kuna baadhi vyenye urefu wa hadi mililita 12. Kipenyo cha vipande hivyo ni mikrometa kadha. Madini
hayo yanakaribiana na madini ya zoisite (aina ya tanzanite), prehnite,
stilbite, chabazite, tremolite, diopside, quartz, calcite, graphite,
alabandite na wurtzite.
"Madini
haya mapya yametambuliwa na taasisi inayoyapa majina madini, IMA CNMNC
(2016-042), na kupewa jina linalotokana na eneo yalipogunduliwa kwa
heshima ya wachimba migodi wa eneo hilo wa zamani, wanaoishi na
wanaofanya kazi," makala ya wataalamu hayo inasema. "Wilaya ya
Merelani imekuwa maarufu tangu mwishoni mwa miaka ya 1960 kutokana na
aina ya madini ya thamani ya rangi ya samawati kwa jina zoisite
yafahamikayo kama tanzanite, lakini ni eneo muhimu sana kwa wanaotafuta
madini ya kipekee na ni eneo la kusisimua sana kutafuta madini mapya,"
John Jaszczak, mwanafizikia katika Chuo Kikuu cha Kiteknolojia cha
Michigan, na aliyeongoza katika kuandika makala kuhusu ugunduzi wa
madini hayo anasema. Madini hayo yalitambuliwa mara ya kwanza
mwaka 2012 na Simon Harrison na Michael Wise, bila wataalamu hao
kuyafahamu vyema, pale walipogundua vitu vilivyoonekana kama nyaya ndogo
zilizokuwa zimedunga na kuingia ndani ya vipande vya madini ya
chabazite. Baadaye uchunguzi zaidi ulifanywa na ikagunduliwa kwamba yalikuwa madini tofauti.
Dawa ya Mpango wa Uzazi kwa Wananume
Dawa inayotolewa kwa njiya ya sindano imetajwa kama mafanikio makubwa ya njiya ya mpango wa uzazi miongoni mwa wanaume.Watafiti kutoka Marekani wamesema dawa hiyo imefikia asili mia 96 ya mafanikio baada ya kufanyiwa majaribio miongoni mwa wanaume 270.Kati ya wanaume hao ni wanne pekee walioweza kuwafanya wenzi zao kutunga mimba. Hata hivyo dawa hiyo imeripotiwa kuwa madhara mengi miongoni mwa wanaume ikiwemo vipele usoni na kuwa na usununu. Watafiti wamekua wakitafuta dawa ya kupanga uzazi ya wanaume kwa miaka 20.
Wataalamu hao wamekua wakitafuta jinsi ya kupunguza idadi ya manii bila kusababisha madhara ya uzazi. Kimaumbile wanaume hutoa manii kila wakati na wanasayansi wamekua wakitaka kupunguza idadi kutoka milioni 15 hadi milioni moja. Utafiti wa dawa hii ulilenga wanaume kati ya umri wa miaka 18 hadi 45, na walio na uhusiano na mwenzi mmoja wa kike. Walishiriki kwenye utafiti huo kwa mwaka mmoja. Walidungwa sindano hiyo na kupunguza idadi ya manii hadi milioni moja. Kisha hawakupokea dawa hiyo ili kubaini kasi ya kuongezeka kwa manii yao hadi milioni 15. Baadhi walisema iliwachukua mwaka mmoja kabla ya idadi kamili na inayotakikana kurudi. Baadhi ya madhara kama vile mfadhaiko, usununu, vipele usoni na maumivu ya misuli yalisababisha wanaume 20 kujitoa kwenye utafiti. Mtafiti mkuu wa dawa hii Dkt. Festin amesema wanaangazia njiya nyingine ya kuboresha dawa hiyo ikiwemo kuiotoa kama mafuta. (Source: BBC)
Saturday, October 15, 2016
Subscribe to:
Posts (Atom)