MENU

Wednesday, November 2, 2016

Africa Kusini: Maandamano yanaendelea muda huu

Kiongozi wa Chama cha EFF, Julius Malema anaendesha maandamano leo yasiyo na kikomo ili kumng'oa madarakani Rais Zuma. Wanashinikiza Rais Zuma ajiuzulu sababu ya kashfa za Ufisadi zinazomkabili. Baadhi ya barabara zimefungwa katika jiji la Pretoria. Maandamano hayo yasio na kikomo yameanzia Church Square katikati ya jiji la Pretoria. Julius Malema akiwa anawahutubia wafuasi wake mbele ya Mahakama Kuu Pretoria aliwaambia kuwa maandamano yatamaliza pindi watakapojisikia kuondoka, lakini hawatakuwa na nia hiyo ya kuondoka. Na pia amewahataadharisha Polisi kutoingilia maandamano yao, amewaambia kazi yao ni kuhakikisha wanapatiwa usalama na si vinginevyo. Amesema hana haja ya kuomba kibali cha maandamano kutoka Polisi au Mahakamani kwani ni haki yake kisheria. 




Hapo awali, Malema aliwaambia Polisi yeye kama Julius Malema Kazi yake nikuandaa Maandamano na kuhakikisha yanafanyika na Polisi kazi yao ni kuwalinda. Maandamano yameanza rasmi leo tarehe 2016 November 02 kuanzia saa 12 za asubuhi mpaka hapo Zuma atakapo achia nchi. Amesema uhuru wa Afrika Kusini haukupatikana kirasihi halafu yeye Zuma aje waibie rasilimali zao, wakati watu wengi waliuwawa kupigania uhuru.

No comments: