MENU
Tuesday, August 30, 2016
Prof. LIPUMBA ALILIA KURUDI UENYEKITI-CUF
Jana baadhi ya viongozi wa Chama cha Wananchi (CUF) walikutana mjini Zanzibar kujadili tukio lililotokea katika Mkutano Mkuu wa chama hicho uliofanyika siku kadhaa nyuma ambapo katika kikao hicho baadhi ya wanachama wa chama hicho walivuliwa uanachama huku wengine wakisimamishwa kwa muda usiojulikana. Wabunge wa wili wa CUF Maftaha Abdallah Nachuma wa Mtwara Mjini na Magdalena Hamis Sakaya wa Kaliua wamevuliwa uanachama kwa kile kilichoelezwa kuwa waliunga mkono vurugu zilizotokea wakati wa mkutano mkuu wa chama hicho . Kwa upande mwingine Prof. Lipumba amesimamishwa uanachama kwa muda usiojulikana.
Taarifa zilizotolewa jioni hii na chama hicho ni kuwa, Julius Mtatiro ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa CUF kwa muda hadi hapo zoezi la kumchagua mwenyekiti litakapofanyika tena. Kufuatia taarifa hiyo, Prof. Lipumba ameibuka na kusema kuwa yeye ndiye mwenyekiti halali wa chama hicho. Aidha, ameeleza kuwa anamtambua Mtatiro kama Mjumbe wa Mkutano Mkuu nafasi aliyompa yeye na wala si mwenyekiti wa chama.
Akizungumzia kuhusu kujiuzulu kwake katika kituo cha ITV, Prof.Lipumba alisema ni kweli kuwa alijiuzulu lakini aliandika barua kwa Katibu wa Chama kutengua uamuzi huo ndiyo sababu yeye nu mwenyekitu wa CUF. Akizungumzia kikao kilichofanyika jana Zanzibar, Prof. Lipumba alisema hatambui maamuzi yoyote ya kikao hicho kwa sababu kuna viongozi kama Naibu Katibu Mkuu Bara, Magdalena Sakaya, hakuwepo kwenye kikao hicho, hivyo maamuzi ya kikao hicho ni batili.
Labels:
HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment