Fursa: Mafunzo ya Ujasiliamali
Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF)
ikishirikiana na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP/UNEP
inaandaa Kongamano la siku moja kuhusu KILIMO BIASHARA katika KANDA YA
ZIWA litakalofanyika Jijini Mwanza siku ya Jumamosi tarehe 27/8/2016
katika Ukumbi wa ROCK CITY MALL ghorofa ya tatu kuanzia saa mbili na
nusu (2:30) asubuhi.
ESRF ilifanya utafiti na kisha kufanya majaribio
katika wilaya sita na kubaini fursa nyingi katika sekta ya kilimo
biashara hususani kilimo cha kisasa “smart farming”. Kwa kulitambua hilo
ESRF ikishirikiana na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa
UNDP/UNEP inaandaa Kongamano la kuelimisha wadau juu ya fursa zilizopo
kwenye kilimo cha kisasa (smart farming)
Kutakuwa na MADA mbalimbali zitakazowasilishwa na
wataalam na wadau waliofanikiwa katika Kilimo Biashara. Mada hizo
zinajumuisha;
- Shamba Kitalu na Ujasiliamali (Green House & Entrepreneurship)
- Kilimo cha malisho ya mifugo (Hydroponic fodder)
- Kilimo cha mbogamboga bila kutumia udongo na ufugaji wa samaki (Hydroponic vegetable and Aquaponic)
- Ufugaji wa kisasa wa samaki katika vizimba, mabwawa na matanki (Cage, Pond and Circulative Fish Farming)
- Azolla - chakula cha mifugo na mbolea asilia
- Ufugaji wa kisasa wa nyuki
- Ufugaji bora wa kuku
Wanawake na vijana wanahimizwa kuhudhuria kwa wingi.
Watakaopenda kuhudhuria wanatakiwa kuthibitisha
ushiriki wao kabla ya tarehe 26/8/2016 kwa kutuma ujumbe mfupi wa
maandishi (sms) kupitia namba 0626645245 na 0627991530 au barua pepe
kilimo@esrf.or.tz (Kongamano hili ni bure na washiriki watajigharimia
gharama nyingine
No comments:
Post a Comment