Dar es Salaam. Hospitali ya Aga Khan Dar es Salaam imekuwa ya kwanza nchini kupewa hadhi ya kimataifa baada ya jopo la wakaguzi wa afya kutoka Marekani kuthibitisha imekidhi vigezo zaidi ya 1,000 vya kutoa huduma bora.
Ukaguzi huo umefanywa na wataalamu hao wiki iliyopita kwa siku nne na kuiweka hospitali hiyo miongoni mwa tisa Afrika zenye hadhi hiyo.
Mkurugenzi wa Wauguzi wa Aga Khan, Lucy Hwai aliwaambia wanahabari jana kuwa mbali na kupata hadhi ya kimataifa, hospitali hiyo imekabidhiwa cheti maalumu kutoka Kamisheni ya Viwango vya Afya vya Kimataifa (JCI).
Mkurugenzi wa Huduma za Afya Aga Khan, Dk Mustaafa Bapumia amesema baada ya kupata cheti hicho, hospitali hiyo itaingia kwenye mfumo wa JCI na kuhakikisha wanazidi kuboresha huduma za afya ili wasipokonywe hadhi hiyo.
No comments:
Post a Comment