AFYA: Apunguza unene baada ya kuambiwa alipie siti mbili kutokana na Unene
PICHA: Ross Garder (Kabla na baada ya kupunguza unene)
Mr Gardner aliyekuwa mfanyakazi katika Mgahawa anasema ''Sikutamani kuendelea kuwa na hali ile ya unene, nilijiogopa hadi mimi mwenyewe, Mama yangu alinisihi sana nipunguze kula na nifanye mazoezi ila sikujua nianzie wapi''.
Anasema wajomba zake walimshauri amuone daktari maana alikuwa anazidi kuwa mnene. Daktari alimuambia kuwa akiendelea kulakula angelikuwa mfu muda si mrefu. ''Mara moja nikaanza kuacha kutumia vilezi na kuvuta sigara na nikaanza kuhudhuria kliniki ya ushauri kuhusu vyakula vya kupunguza unene.''. Bwana Gardner kwa sasa anawasaidia wengine kupunguza tatizo la unene.
Anasema hatasahau siku moja alipotakiwa kukata tikiti mbili za ndege kwakuwa yeye alikuwa mnene na ndipo alipoanza kutafuta namna ya kupunguza unene wake. Yote yanawezekana.
No comments:
Post a Comment