MENU

Wednesday, July 13, 2016

Uholanzi: Serikali yafunga Magereza 19 kutokana na Uhaba wa Wafungwa



 

Kupungua kwa uhalifu imeilazimisha serikali ya Uholanzi kuangalia kufunga zaidi ya magereza 19 miaka michache ijayo kwakukosekana kwa wafungwa

Kupungua kwa idadi ya matukio ya wizi inailazimisha serikali ya Uholanzi kufunga magereza kutokana na kukosekana kwa wafungwa. Kutonana na Ard van der Steur, Waziri wa Ulinzi na Sheria, Mahakimu wanatoa hukumu za muda mfupi na hivyo kusababisha watu kukaa jela muda mfupi. Lakini pia kumekuwa na punguzo la uhalifu. Waziri huyo amesema kutokana na kupungua kwa wafungwa magerezani maana yake hata wafanyakazi wapatao 1,900 pia itabidi wakose vibarua vyao. Amesisitiza kuwa kufungwa kwa magereza ni lazima maana gharama za kuhudumia magereza ni kubwa ijapokuwa hakuna wafungwa.





No comments: